IQNA

Ushauri kwa wasomi katika maonyesho ya Qur’ani Tehran

13:36 - August 10, 2011
Habari ID: 2168385
Waandishi wa makala za Qur’ani kwa ajili ya Shahada ya Uzamivu-Phd- watapokea ushauri wa jumla na maalumu kuhusu marejeo ya Qur’ani na namna ya kufanya utafiti katika Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qur’ani mjini Tehran.
Kwa mujibu wa mkuu wa kitengo cha utafiti katika maonyesho hayo Bw. Mohammad Ali Hashemzadeh, watafiti watapata fursa ya kupitia miradi ya utafiti iliyotekelezwa huko nyuma. Amesema wasomi hao wa shahada ya uzamivu watapewa miongozo kuhusu namna ya kuandika makala na tasnifu zao.
Amesema kuna haja ya kutumia marejeo mapya ili kuboresha makala za utafiti. Ameongeza kuwa mada mpya za utafiti pia zitaarifishwa. 839271
captcha