IQNA

"Mwamko wa Kiislamu" wajadiliwa katika maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani

17:24 - August 13, 2011
Habari ID: 2169853
Kikao maalumu cha mwamko wa Kiislamu kimefanyika Agosti 11 katika maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu Tehran.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Abu Sharif, mwakilishi wa wa harakati ya Jihad Islami ya Palestina katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Amefafanua kuhusu matukio ya hivi karibuni katika eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika na athari zake huko Palestina.
Kikao hicho kimejadili kwa kina sababu na matokeo ya mwamko wa Kiislamu katika baadhi ya nchi za Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika pamoja na masuala ya Palestina.
Kitengo cha 'Mwamko wa Kiislamu' katika Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani y Tehran huandaa vikao maalumu kila siku katika maonyesho hayo ambayo yanaendelea katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini RA mjini Tehran.
841730
captcha