IQNA

Vitabu kadhaa vya Kiislamu kwa lugha ya Kireno vyaonyeshwa katika maonyesho ya Qur'ani

17:30 - August 13, 2011
Habari ID: 2169869
Jumuiya ya Urafiki ya Iran na Brazil inaonyesha vitabu kadhaa vya Kiislamu kwa lugha ya Kireno katika maonyesho ya Qur'ani Tukufu hapa mjini Tehran.
Vitabu hivyo vimetarjumiwa na Sheikh Talib Khazraji. Mfumo wa kijamii katika Uislamu, swala katika Uislamu, masomo kutoka Nahjul Balagha, wilaya na al-Mahdi pamoja na masomo kutoka Qur'ani Tukufu ni baadhi ya vitabu vinavyoonyeshwa katika maonyesho hayo na jumuiya iliyotajwa.
Vitabu hivyo vimechapishwa na Kituo cha Kiislamu cha Brazil.
Mbali na Ureno kwenyewe, lugha ya Kireno pia huzungumzwa kama lugha rasmi nchini Brazil na nchi kadhaa za Kiafrika.
Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani yanayoendelea mjini Tehran yamepangwa kukamilika tarehe 26 mwezi huu wa Agosti. 841737
captcha