Hujjatul-Islam Kadhim Sidiqi Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo hapa mjini Tehran amesema maandamano katika miji tofauti ya Uingereza yanaonyesha uhakika wa ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyosisitiza na Imam Khomeini MA kwamba, mwishoni wanyonge watawashinda madhalimu.
Kuhusu sababu ya kuanza maandamano katika baadhi ya nchi za Ulaya ikiwemo Uingereza, Hujjatul-Islam Sidiqi amesema, maandamano yanayojiri sasa huko Ulaya ni matokeo ya jinai zilizofanywa na baadhi ya viongozi wa nchi za Magharibi katika nchi nyinginezo.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesisitiza kwamba, baadhi ya nchi za Magharibi ikiwemo Uingereza zinakalia kwa mabavu nchi nyinginezo na fedha wanazotumia huko zinatokana na kodi za wananchi, suala ambalo limepelekea kuzuka malalamiko ndani ya nchi hizo.
841655