Mhadhiri wa Kituo cha Kiislamu cha Hamburg nchini Ujerumani Hujjatul Islam Ismail Gandomkar amesema katika kikao kilichochunguza wimbi la kuchomwa moto Qur'ani kilichofanyika jana katika Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qur'ani mjini Tehran kwamba kuvunjiwa heshima Qur'ani ni sawa na kuvivunjia heshima vitabu vya Tauratu na Injili, kwa msingi huo kuna udharura wa kubuniwa baraza kuu la dini ambalo litapiga marufuku vitendo vya aina yoyote ile vinavyovunjia heshima dini na vitabu vitakatifu.
Ustadh Gandomkar ambaye alikuwa akizungumzia matukio ya kuchomwa moto Qur'ani na propaganda chafu dhidi ya Uislamu nchini Marekani, amesema vitendo hivyo vya kuchomwa moto Qur'ani ni sehemu ya mpango wa muda mrefu wa kuuhujumu Uislamu unaotekelezwa na Wazayuni na Marekani pamoja na kasisi mmoja mwenye asili ya Ujerumani ambaye alichoma moto kitabu hicho kitakatifu huko Florida.
Amesema maadui hao wameelewa kwamba Qur'ani Tukufu ndio chanzo na marejeo ya kuaminiwa zaidi katika medani za kimataifa, kwani dini za Ukristo na Uyahudi hazina jipya. Amesisitiza kuwa kuchoma moto Qur'ani ni suluhisho la matatizo yao na watu hao wanapawa kujibu hoja za kimantiki za kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu. 842783