IQNA

OIC yalaani upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi

15:07 - August 15, 2011
Habari ID: 2170694
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imelaani vikali mpango wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kupanua ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Profesa Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC amesema kuwa, kuendelea ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Palestina kunazidi kuvuruga amani na usalama wa Mashariki ya Kati. Katibu Mkuu wa OIC amesisitiza kwamba, Quds ni eneo lisilotenganishika na ardhi za Palestina.
Ameongeza kuwa, hatua za utawala wa Kizayuni wa Israel za kubadilisha muundo wa kijiografia na kijamii wa Quds Mashariki na kulitenganisha eneo hilo na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni haramu na kwamba, zinakinzana wazi na sheria za kimataifa.
Kwa mara nyingine tena, Katibu Mkuu wa OIC ameitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za maana za kuhitimisha uvamizi wote wa utawala dhalimu wa Israel huko Palestina.843070
captcha