IQNA

Kikao cha dharura cha OIC kuhusu Somalia kufanyika wiki hii

15:35 - August 15, 2011
Habari ID: 2171310
Kikao cha dharura cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC kuhusu baa la njaa nchini Somalia kitafanyika wiki hii mjini Istanbul Uturuki.
Kikao hicho cha Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi wanachama wa OIC kitafanyika Jumatano ya wiki hii na kitajadili hali ya kibinaadamu na baa la njaa linaloikabili Somalia.
Taarifa ya OIC imebainisha kwamba, lengo hasa la kikao hicho ni kukusanya nguvu zaidi za kukabiliana na ukame pamoja na baa la njaa katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, juhudi za kieneo na kimataifa za kuwasaidia wananchi wa Somalia zinaendelea kushuhudiwa ambapo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana ilituma shehena ya tatu ya misaada ya kibinadamu kwa wananchi wa Somalia.
Iran imetangaza kuwa, kufikia mwishoni mwa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani itakuwa imetuma misaada ya dola milioni 25 huko Somalia.
843439


captcha