IQNA

Semina ya Bima ya Kiislamu yafanyika Nigeria

11:56 - August 17, 2011
Habari ID: 2172236
Shirika la African Alliance Insurance PLC limeandaa semina ya siku moja kuhusu Bima ya Kiislamu ya Takaful huko Kano, Kaskazini mwa Nigeria.
Semina hiyo iliyofanyika Agosti 15 iliwashirikisha wadau wa bima katika eneo hilo.
Mkuu wa shirika hilo Alphonse Okpor amesema lengo la semina hiyo ni kufuta ile dhana potofu kuwa bima ni haramu katika Uislamu. Amesema, ‘mfumo wa bima ya Kiislamu ya Takaful umekuwa ukitumiwa katika nchi za Kiislamu kwa muda mrefu’. Amesema wafanyakazi wa shirika lake wametembelea Saudi Arabia na Malaysia ili kujifunza namna mfumo wa bima ya takaful unavyoendeshwa.
Naye Malam Musa Abdullahi wa Kituo cha Masomo ya Mfumo wa Fedha wa Kiislamu Malaysia amesema mfumo wa Takaful ulitumika tokea zama za awali za Uislamu. 844527
captcha