IQNA

Siku ya Quds, nembo ya mapambano ya Waislamu mbele ya Wazayuni

12:32 - August 20, 2011
Habari ID: 2173620
Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesema kuwa, Siku ya Kimataifa ya Quds ni siku ya kuonyesha kusimama kidete Waislamu katika kukabiliana na utawala ghasibu wa Israel.
Huku akiasharia hatua ya Imam Khomeini MA, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kuitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani kila mwaka kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds, Ayatullah Ahmad Jannati amesema, Siku ya Quds ni siku ambayo Waislamu wote na wapenda haki duniani husimama kidete dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake Ayatullah Jannati ameashiria hali ya mgogoro wa Somalia na kuzikosoa baadhi ya nchi za Magharibi na taasisi za kimataifa kwa kutoipa umuhimu hali ya njaa inayowakabiliwa wananchi wa Somalia.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya jana mjini Tehran ametoa mwito kwa nchi za Kiislamu kufanya hima ya kuwasaidia ndugu zao wa Somalia.
846018
captcha