IQNA

Al-Azhar yalaani mashambulio ya utawala wa Kizayuni Gaza

14:59 - August 21, 2011
Habari ID: 2174479
Ahmad Tayyib Sheikh wa al-Azhar nchini Misri Ijumaa iliyopita alitoa taarifa akilaani vikali mashambulio ya utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
Amelaani mashambulio hayo ambayo pia yalikiuka mipaka ya Misri na wakati huohuo kuwashukuru askari usalama wa Misri kwa kulinda usalama wa mpaka wa nchi hiyo katika eneo la jangwa la Sinai. Ametoa mkono wa pole kwa familia za wahanga wa hujuma hiyo ya Israel na kuyataka makundi yote ya kisiasa ya Misri kuweka kando tofauti zao ili kupambana na adui wao wa pamoja ambaye ni utawala wa Kizayuni.
Usiku wa siku ya Alkhamisi kuamkia Ijumaa utawala ghasibu wa Israel ulifanya hujuma kali katika Ukanda wa Gaza ambapo ulishambulia kwa mabomu na kubomoa majengo muhimu ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas. Watu wapatao 7 waliuawa shahidi na wengine 17 kujeruhiwa katika hujuma hiyo ya kinyama.
Utawala huo ulifanya hujuma nyingine kama hiyo katika ardhi ya Misri ambapo uliwaua askari 3 wa kulinda usalama wa nchi hiyo. Utawala ghasibu wa Israel unadai kuwa ulifanya hujuma hiyo kujibu mashambulio yaliyofanywa dhidi ya basi moja la abiria katika eneo la Ilat ambapo Wazayuni 8 waliuawa. 846703
captcha