Balozi Shalom Kohen na wafanyakazi wa ubalozi wa utawala wa Kizayuni wametakiwa kuondoka haraka kwa mujibu wa sheria za Kimataifa.
Rais Hugo Chavez wa Venezuela amelaani vikali hujuma ya utawala wa Kizayuni dhidi ya ukanda wa Ghaza na kutaja jinai hiyo kuwa mauaji ya umati.
Katika kipindi cha siku nne zilizopita Wapalestina wasiopungua 16 wameuawa katika hujuma za anga za utawala wa Kizayuni huko Ghaza.
Mushir al Masri, msemaji wa mrengo wa mabadiliko na mageuzi katika bunge la Palestina amesema kwamba, Israel inakusudia kuamsha hasira za Wapalestina kwa kushambulia mara kwa mara Gaza, kuua na kuwakamata Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huku ikiendeleza siasa zake za kuiyahudisha Quds na kuchimba mashimo chini ya Msikiti wa al Aqsa.
Ameongeza kuwa, Israel inashambulia Gaza ili kujaribu kukwepa mgogoro unaotokota ndani ya utawala huo, lakini Hamas na makundi ya muqawama hayataruhusu suala hilo kuendelea.
847301