IQNA

Ihsanouglu ataka kusimamishwa mashambulio ya Wazayuni Gaza

14:45 - August 24, 2011
Habari ID: 2175975
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC Ekmeleddin Ihsanoglu ametoa taarifa akitaka kusimamishwa mara moj jinai na mashambulio yanayoendeshwa na utawala haramu wa Israel dhidi ya raia wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza.
Katika taarifa hiyo Ihsanouglu ameitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka ili kuingilia kati na kusimamisha jinai zinazofanywa na utawala huo dhidi ya Wapalestina wasio na wa kuwalinda.
Amesema mashambulio hayo yanayopelekea kuuawa na kujeruhiwa watu wasio na hatia wakiwemo wanawake na watoto wadogo, licha ya kuwa yanakiuka sheria za kimataifa pia yanavuruga uthabiti wa Mashariki ya Kati.
Katibu Mkuu wa OIC ametaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya utawala haramu wa Israel ili kuulazimisha kusimamisha mara moja mzingiro uliouwekea Ukanda wa Gaza. 848426
captcha