IQNA

Imam wa Quds Tukufu:

Siku ya Quds ni wito wa mapambano ya jihadi dhidi ya ubeberu

17:56 - August 24, 2011
Habari ID: 2176407
Imamu wa Msikiti wa Quds Tukufu katika mji wa Sidon nchini Lebanon amesema kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds ni siku ya kuwalingania Waislamu vita vya jihadi na mapambano dhidi ya mabeberu na kuwa na mshikamano zaidi.
Sheikh Mahir Hamoud amesema kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds ni hatua muhimu katika njia ya kuwatetea wananchi wanaokandamizwa mbele ya mabeberu kwa moyo uliojaa imani na yaqini kamili kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu SW itatimia.
Naye Ahmad Zein, Mwenyekiti wa Baraza la Maulamaa wa Lebanon amesema kuwa haifai katika kipindi hiki ambapo madola ya kibeberu yanauunga mkono utawala wa Kizayuni wa Israel na kuusaidia kwa hali na mali, kuwaacha peke yao wananchi wa Palestina.
Sheikh Ikrima Sabri, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Quds Tukufu amesema Siku ya Kimataifa ya Quds imehuisha kadhia ya Palestina katika nyoyo za vizazi vijavyo, kwa msingi huo kuna udharura wa kusisitiza juu ya umuhimu wa suala hilo kwa ajili ya kuweza kufikia lengo tukufu la kuikomboa Quds Tukufu. 849034

captcha