Suala la Palestina na kukaliwa kwa mabavu Beitul Muqaddas, ni mgogoro wa kihistoria wa muda mrefu kati ya Waislamu na walowezi wa Kizayuni, mgogoro ambao umekuwa ukiongezeka kila mwaka.
Akibainisha suala hilo, Mahir Tahir, mmoja wa maafisa wa ngazi za juu wa Chama cha Ukombozi wa Palestina PLO amesema kuwa pendekezo lililotolewa na Imam Khomeini (MA) la kuadhimishwa kila mwaka Siku ya Kimatifa ya Quds katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, lilitokana na ukweli kuwa mji mtakatifu wa Quds ni mji ulio na utambulisho wa Kiarabu na Kiislamu. Amesema jambo hilo linazingatiwa sana na Waislamu pamoja na Wakristo na ndio maana wakawa wanashiriki kwa wingi katika maandamano hayo ambayo hufanyika kila mwaka kote duniani.
Wakati huohuo amesema kwamba licha ya uharibifu na hujuma kubwa inayofanywa na Wazayuni dhidi ya mji huo lakini Waislamu na Waarabu hawachukui hatua za kutosha kwa ajili ya kupambanana hujuma hiyo.
Mahir Tahir amesema licha ya kuwa asilimia 84 ya Beitul Muqaddas hivi sasa inakaliwa na walowezi wa Kizayuni lakini Waislamu na Waarabu hawajachukua hatua yoyote ya maana ya kukabiliana na hali hiyo ya kusikitisha.
Amesema, Wazayuni ambao wamekuwa wakitekeleza siasa zao kwa mpangilio maalumu hivi karibuni watauchukua mji huo wote na kuutangaza kuwa mji mkuu wao. 849082