Mafanikio na matunda ya Siku ya Quds ambayo ilitangazwa rasmi na mwanzilishi wa mfumo wa Kiislamu wa Iran Imam Khomeni (MA), yanaimarika na kunawiri zaidi mwaka hadi mwaka katika ulimwengu wa Kiislamu.
Mfano wa matunda hayo ni ushindi mkubwa wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah dhidi ya wavamizi wa Kizayuni nchini humo na vilevile ya Hamas huko katika Ukanda wa Gaza.
Hayo yamesemwa na Ghazi Huneini, Mkuu wa Harakati ya Umoja ya Lebanon. Amesema wananchi wa Lebanon kama walivyo wenzao katika sehemu nyingine za dunia, wanaitambua Siku ya Quds kuwa siku ni tukufu. Amesema katika siku hii Waislamu, Wakristo na hata Mayahudi hushirikiana kwa karibu kuiadhimisha siku hii ili kufikia lengo moja dhidi ya walowezi wa Kizayuni.
Huneini amewataka walimwengu wote kuliondoa donda hilo la saratani katika Mashariki ya Kati ili kuwawezesha Waislamu, Wakristo na Mayahudi kuishi pamoja kwa amani katika eneo hilo. Amesema Palestina ni kituo cha amani, umoja na kukutana pamoja staarabu tofauti za jamii ya mwanadamu na sio kituo cha vita vya staarabu hizo. 849122