IQNA

Siku ya Quds inaimarisha Mwamko wa Kiislamu

14:33 - August 27, 2011
Habari ID: 2177147
Balozi wa Palestina mjini Tehran amesema kuadhimishwa Siku ya Kimataifa ya Quds ni hatua muhimu katika kuimarisha mwamko wa Kiislamu.
Akizungumza na IQNA, Salah Zawawi amesisitiza kuwa, leo Waislamu kote duniani wanaunga mkono kadhia ya kukombolewa Quds Tukufu.
“Quds ni mji mkuu wa Palestina na una nafasi muhimu katika ulimwengu wa Kiislamu”, ameongeza.
Zawawi amesema, kuikomboa Palestina si jukumu la Wapalestina pekee. “Ni jukumu la Waarabu na Waislamu wote pamoja na wapenda uhuru kote duniani kupigania ukombozi wa Palestina. Hakuna shaka kuwa kukombolewa Palestina kutakuwa na nafasi muhimu ya kustawisha umoja wa Kiislamu duniani”.
Ameashiria ubunifu wa Imam Khomeini MA wa kuitaja Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa ni Siku ya Quds na kusema, “Hayati Imam alitazama kadhia ya Palestina kama suala muhimu zaidi la ulimwengu wa Kiislamu”.
Katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, mamilioni ya Waislamu wamejitokeza katika maandamano kote duniani wakitaka utawala haramu wa Israel usitishe ukaliaji mabavu wa Palestina.
849291
captcha