Watunisia walijitokeza katika maeneo mbalimbali nchini humo katika Siku ya Quds na kutangaza mfungamano wao na wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina huku wakilaani vikali utawala wa Kizayuni wa Israel. Wakati wa dikteta aliyetimuliwa Zein al Abidine ben Ali, Watunisia hawakuwa na haki ya kuadhimisha siku ya Quds.
Akizungumza na kanali ya televisheni ya al Alam, Khalil Shahin mtaalamu wa masuala ya kisiasa wa Tunisia amesema, ‘Siku ya Quds ni tukio muhimu katika Ulimwengu wa Kiislamu ambapo mataifa yote hupata fursa ya kuwaunga mkono Wapalestina wanaodhulumiwa’.
Amesema njama za utawala bandia wa Israel za kuuyahudisha mji wa Quds na kufuta utambulisho wa Kiislamu na Kipalestina wa mji huo ni jambo ambapo linalowajibisha Waislamu wote duniani kuzingatia kadhia ya Quds.
849946