IQNA

Maandamano ya Siku ya Quds nchini Nigeria

11:33 - August 28, 2011
Habari ID: 2177842
Waislamu nchini Nigeria wamejiunga na wenzao duniani katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya Quds katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi tukufu wa Ramadhani.
Maandamano makubwa yamefanyika katika miji mbalimbali ya Nigeria yakishirikisha maelfu ya Waislamu . Maandamano makubwa zaidi yamefanyika katika miji ya Kano na Kaduna kaskazini mwa Nigeria. Maandamano hayo yameandaliwa na Harakati ya Kiislamu ya Nigeria inayoongozwa na Sheikh Ibrahim Zakzaki.
Waandamanji walikuwa wamebeba mabango yaliyokuwa yameandikwa “Mauti ya Israel” na “Mauti kwa Marekani”. Aidha waandamanaji waliokuwa wamebeba bendera za Palestina wameteketeza moto bendera za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Waandamanaji hao pia walikuwa wamebea picha za Imam Khomeinia RA, Imam Khamenei na Kiongozi wa Hizbullah Sayyid Nasrullah.
Baadhi ya Waislamu wa Nigeria wametangaza kuwa wako tayari kujiunga na Wapalestina katika kupigania ukombozi wa mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na Wazayuni. Wamesema kuwa Quds ni ya Waislamu wote. Waandamanaji Nigeria pia wamelaani mauaji yanayoendelea kutekelezwa na utawala wa Kizayuni huko Ghaza.

850634
captcha