IQNA

Kurejea kwenye utambulisho wa Kiislamu ni chanzo kikuu cha mapinduzi ya Libya

11:49 - August 28, 2011
Habari ID: 2177914
Sayyid Sadr ad-Deen Qubanchi, Imam wa Swala ya Ijumaa ya mji mtakatifu wa Najaf amesema kwamba sababu na chanzo kikuu cha kufanyika mapinduzi ya Libya ni hamu ya wananchi wa nchi hiyo ya kurejea kwenye utambulisho wao wa Kiislamu.
Ameongeza kuwa hii leo mataifa yanafanya mapinduzi na harakati za ukombozi kwa jina la dini na Uislamu na wala sio kwa jila la usoshalisti. Akizungumza katika swala ya Ijumaa ya Najaf, Hujjatul Islam wal Muslimin Qubanchi amesema kuwa kuna sababu nyingi zilizopelekea kufanyika mapinduzi ya Libya muhimu kati ya hizo ikiwa ni hamu ya wananchi ya kutaka kurejea kwenye Uislamu wao. Amewapongeza wananchi Waislamu wa Libya kwa moyo wao wa kupigana na kumshinda dikteta Mummar Gaddafi na kuongeza kuwa Qaddafi alikuwa muungaji mkono mkubwa wa dikteta mwenzake wa Iraq Saddam Hussein katika kipindi cha utawala wake wa miaka 42 nchini Libya.
Imam wa Swala ya Ijumaa ya Najaf amewataka Walibya baada ya kupata ushindi huo muhimu kuimarisha umoja na kujiepusha na kila jambo linalochochea chuki na uadui kati yao.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake Qubanchi amesema kuwa utawala haramu wa Israel unataka kutekeleza mpango na njama hatari ya kuimarisha satuwa yake katika eneo zima la Mashariki ya Kati kupitia miradi ya kibiashara na mbinu za kisiasa.
Mwishoni mwa hutuba yake Sayyid Qubanchi amesema kwamba pendekezo lililotolewa na Imam Khomeini (MA) mwanzilishi wa mfumo wa Kiislamu wa Iran kwamba Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani iadhimishwe kama Siku ya Quds ni pendekezo la Kiislamu na kimataifa moja kwa moja na linalovuka mipaka yote ya kijografia, kieneo na kikabila. 850444
captcha