Serikali ya Algeria imetangaza kuwa hakuna uwezekano wowote kwamba Gaddafi na wanawe waliokuwa katika magari ya deraya wamekimbilia nchini Algeria.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria amesema kuwa habari zinazodai kuwa gari iliyokuwa imembeba Gaddafi na familia yake imeingia nchini humo, hazina kweli wowote.
Vyama vya upinzani vya Libya pia vimetangaza kuwa hakuna taarifa yoyote kuhusu mahala alipo Muammar Gaddafi na wanawe. 851115