Ripoti zinasema kuwa walioshiriki katika kikao hicho cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Kiarabu walishusha chini bendera ya utawala wa Gaddafi na kupandisha juu bendera ya wanamapinduzi wa nchi hiyo. Mawaziri hao walikutana jana katika kikao cha dharura kuchunguza hali ya Libya.
Mwakilishi wa Baraza Kuu la Mpito la Libya Mahmoud Jibril ambaye pia ameshiriki katika kikao hicho amesisitiza juu ya kusaidiwa kifedha baraza hilo.
Mapigano ya kuuondoa kabisa madarakani utawala wa Muammar Gaddafi nchini Libya yanaendelea na dikteta huyo hajulikana aliko. 851598