IQNA

Baadhi ya nchi za Kiislamu zaadhimisha Idil Fitri leo

14:59 - August 30, 2011
Habari ID: 2179117
Nchi nyingi za Kiarabu na nyengine kadhaa zisizokuwa za Kiarabu leo zinasherehekea sikukuu ya Idil- Fitri baada ya kumalizika Funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Waislamu katika nchi za Saudi Arabia, Kuwait, Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu, Qatar, Jordan, Sudan, Lebanon, Yemen, Libya, Syria na Palestina leo wanasherehekea Idil-Fitri.
Sikukuu hiyo inasherehekewa leo pia katika nchi za Uturuki, Malaysia, Uzbekistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tadjikistan na nchi kadhaa za Ulaya na Marekani.
Hapa nchini Iran na katika nchi nyengine kadhaa ikiwemo Oman na Indonesia Idil-Fitri itaadhimishwa kesho Jumatano.
shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa IQNA linawatakia Waislamu kote duniani sikukuu njema na Idil Fitri.
851187

captcha