IQNA

Libya yaahidi kufungua faili la Musa Sadr

15:02 - August 30, 2011
Habari ID: 2179142
Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon amesema kuwa Libya imeahidi kufungua faili la Imam Musa Sadr aliyetekwa nyara na dikteta Muammar Gaddafi akiwa na wenzake wawili.
Akizungumza hivi karibuni katika kikao cha dharura cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu huko Cairo Misri, Adnan Mansur, Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon amesema kuwa alizungumzia kwa kina udharura wa kufuatilia suala la kutafutwa sehemu alikofichwa mwanazuoni huyo wa Kiislamu alipoonana na Mahmoud Jibril, Mkuu wa Ofisi ya Uandamizi ya Barala la Kitaifa la Libya ambaye pia ni mkuu wa uhusiano wa kigeni wa baraza hilo pambizoni mwa kikao hicho.
Viongozi wawili hao pia walijadili suala la kuanzisha tena uhusiano wa kidiplomasia wa nchi mbili na kuimarisha ushirikiano wa pande hizo katika nyanja zote.
Imam Musa na wenzake wawili, Sheikh Muhammad Ya'qub na Abbas Badr Deen, mwandishi habari, walitekwa nyara nchini Libya tarehe 31 Agosti na hadi leo hatima yao haijulikani. 852228
captcha