Kikao cha 27 cha Kamati ya Kudumu ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Masoko wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirkikiano wa Kiislamu OIC kimepangwa kufanyika tarehe 16 na 17 Oktoba mjini Istanbul, Uturuki.
Kikao hicho cha COMCEC kitaongozwa na Rais Abdullah Gul wa Uturuki.
Miongoni mwa ajenda za kikao hicho ni pamoja na kujadili njia za kuzidisha ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi za Kiislamu na kupambana na umaskini na vilevile kikao cha mawaziri wa uchumi wa nchi za Kiislamu watakaochunguza njia za usafirishaji rahisi wa mizigo ya kibiashara kati ya nchi wanachama.
Mbali ya mawaziri wa uchumi wa nchi wanachama katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC, kikao hicho pia kitahuduriwa na wawakilishi wa taasisi za kiuchumi na kibiashara za Kiislamu na wa jumuiya za kimataifa. 853574