Hamid Ahmadi mmoja wa makamanda wa operesheni za kikosi cha nchi kavu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, baada ya kumalizika awamu ya mwezi mmoja, vikosi vya jeshi hilo Ijumaa hii vitaanza duru mpya ya operesheni dhidi ya kundi la kigaidi la Pijak ili kuwafukuza wanachama wa kundi hilo katika mipaka ya kaskazini magharibi mwa Iran na kwamba operesheni hiyo itaendelea hadi kuliangamiza kikamilifu kundi hilo.
Kamanda Hamid Ahmadi ameongeza kuwa kikosi kilichotajwa kilitoa mwezi mmoja kwa magaidi wa Pijak na kuliainishia masharti mbalimbali kukiwemo kuondoka kikamilifu magaidi hao katika maeneo ya mpakani huko magharibi mwa Iran na kujiepusha kundi hilo na utekelezaji wa oparesheni yoyote ya kigaidi chini ya upatanishi wa uongozi wa kieneo wa Kurdistan ya Iraq.
Amesema, licha ya hayo, lakini kundi la kigaidi la Pijak limepuuza ombi hilo na kuamua kufyatua risasi na kuvurumisha makombora yaliyowaua shahidi wanajeshi wawili wa Kikurdi.
854194