IQNA

Iran haipasi kuchukuliwa kuwa adui wa Misri

12:57 - September 05, 2011
Habari ID: 2181523
Mgombea mmoja wa kiti cha rais wa Misri amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haipasi kuchukuliwa kuwa adui wa Misri, bali ni nchi ya Kiislamu iliyo na nguvu kubwa ambayo inafanya juhudi za kueneza ustaarabu na utamaduni wa Kiislamu duniani.
Hayo yamesemwa na Muhammad Salim al-Awa ambaye anatazamiwa kugombea kiti cha rais wa Misri hivi karibuni. Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wasomi pamoja na shakhsia muhimu wa nchi hiyo. Amewataka viongozi wa hivi sasa wa Misri kuamiliana na utawala haramu wa Israel kama adui na sio rafiki.
al Awa amesisitiza umuhimu wa kudumishwa uhusiano wa kirafiki na taifa la Palestina na kuongeza kuwa Iran imekuwa ikiyasaidia kwa hali na mali makundi ya mapambano ya Kiislamu ya Palestina na kuwa kwa msingi huo nchi hii haipasi kuchukuliwa kuwa adui.
Vilevile amewataka viongozi wa Misri kutazama upya uhusiano wao na Marekani ambayo ni muungaji mkono mkubwa wa utawala haramu wa Israel na kufanya juhudi za kutohitajia misaada ya nchi hiyo ya kikoloni. Amesisitiza kwamba uingiliaji wa Marekani katika masuala ya ndani ya Misri ni jambo lisilokubalika kabisa na kwamba taifa la Misri linapasa kuzingatia tu maslahi ya kitaifa ya nchi hiyo kwa kutegemea raslimali na maliasili zake. 854407
captcha