IQNA

Utawala wa Bahrain watumia silaha za Marekani kuwakandamiza raia

21:59 - September 06, 2011
Habari ID: 2182632
Utawala wa kidikteta wa Bahrain unanunua silaha kutoka Marekani kwa ajili ya kuwakandamiza raia wa nchi hiyo.
Waandamanaji kadhaa Bahrain wameuawa shahidi na kujeruhiwa katika miezi kadhaa ya hivi karibuni kufuatia hatua ya vikosi vya usalama vya nchi hiyo ya kuwanyunyizia gesi ya kutoa machozi raia hao. Mmoja kati ya raia hao waliouawa na vikosi vya usalama vya Bahrain ni Ali Jawad aliyekufa shahidi katika Sikukuu ya Idul Fitr baada ya kufyatuliwa kichwani gesi ya kutoa machozi.
Wananchi wa Bahrain ambao kwa miezi sita sasa wanafanya maandamano ya amani kote nchini humo, wanautaka utawala wa kidikteta wa Aal Khalifa uondoke madarakani, wafungwa wa kisiasa waachiwe huru na marekebisho ya kisiasa yatekelezwe nchini humo.
855676
captcha