Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bait Sheikh Muhammad Hassan Akhtari amesema kuwa mkutano huo utafunguliwa Jumapili ijayo kwa hotuba ya Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran na utamaliza shughuli zake siku ya Jumatano. Amesema wageni 600 kutoka nchi za kigeni na wasomi 400 wa ndani ya Iran watashiriki katika mkutano huo.
Kuhusu malengo ya mkutano huo wa kimataifa Sheikh Akhtari amesema kuwa miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa ni mwamko wa Kiislamu chini ya mafundisho ya Ahlul Bait hususan kwa kutilia maanani hali ya sasa ya kimataifa na wimbi la mwamko wa Kiislamu liliyoyambumba maeneo ya kaskazini mwa Afrika na Mashariki ya Kati.
Mkutano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bait hufanyika mara moja kila baada ya miaka minne ukiwashirikisha wasomi, wanafikra na wanazuoni wa madhehebu ya Ahlul Bait kutoka pembe zote za dunia. 854367