Ayatullah Jannati amesema, Uturuki imejipatia sifa kubwa katika ulimwengu wa Kiislamu kutokana na hatua yake hiyo ya kijasiri.
Hata hivyo Ayatullah Jannati amekosoa hatua ya viongozi wa Ankara ya kuliruhusu shirika la kijeshi la Magharibi NATO kuweka ngao dhidi ya makombora nchini mwao akisema kuwa suala kama hilo linahatarisha usalama wa eneo zima la Mashariki ya Kati.
Kuhusu ukandamizaji unaofanywa na utawala wa Aal Khalifa dhidi ya wananchi huko Bahrain, khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa hapa Tehran amesema, utawala wa kifalme wa nchi hiyo hauwezi kuwafunga mdomo wananchi miaka yote na kwamba njia pekee ya kutatua mgogoro ulioko ni kukubali kutekeleza matakwa ya wananchi wanaoandamana.
857361