IQNA

Wamisri wauonya utawala wa Saudi Arabia

14:44 - September 11, 2011
Habari ID: 2184864
Wananchi wanampinduzi Misri wameushambulia ubalozi wa Saudi Arabia mjini Cairo kutokana na uingiliaji wa nchi hiyo katika masuala ya ndani ya Misri.
Mwanachama mwandamizi wa Harakati ya 'Kifaya' Karima Hafnawi amesema hujuma dhidi ya Ubalozi wa Saudia mjini Cairo ni onyo kali la Wamisri kwa utawala wa Aal Saud usitishe njama zake dhidi ya mapinduzi ya wananchi Misri. Amesema Saudi Arabia inajaribu kutumia ushawishi wake kusimamisha kesi dhidi ya dikteta Husni Mubarak. Ameongeza njama dhidi ya mapinduzi ya wananchi wa Misri inapangwa na Saudi Arabia, Utawala haramu wa Israel na Marekani.
Hivi karibuni Aidh al Qarani ambaye ni miongoni mwa mamufti wakubwa wa Kiwahabi wa Saudi Arabia alitoa mtazamo wa kuchekesha kwa kufananisha kuingia dikteta wa Misri Hosni Mubarak na wanawe wawili mahakamani na jinsi Nabii Yusuf AS na vijana wawili walivyoingizwa jela! 858313
captcha