Marau Amadou Waziri wa Sheria wa Niger amesema kwamba, Saad aliingia Niger jana katika msafara wa watu 9. Ameongeza kwamba msafara huo ilikuwa ukielekea kusini katika eneo la Agadez ambako inaaminiwa kuwa maafisa wa ngazi za juu wa utawala wa Gaddafi wamejificha katika hoteli moja.
Niger pia imethibitisha kwamba majenerali watatu wa ngazi za juu wa utawala wa Gaddafi akiwemo Al Rifi Ali al Sharrif aliyekuwa mkuu wa kikosi cha anga cha Libya pia amewasili katika eneo la Agadez.
Mwana wa Gaddafi Saad mwenye umri wa miaka 37 ni shakhsia aliyekuwa na ushawishi mkubwa katika utawala ulioanguka wa Libya.
859260