IQNA

Utawala wa Israel mhasirika mkuu wa mapinduzi ya Kiislamu katika eneo

18:38 - September 14, 2011
Habari ID: 2187109
Katika toleo lake la hapo jana Jumanne, gazeti la Kurier la nchini Austria limesema kuwa utawala haramu wa Israel ndio mhasirika mkuu wa mapinduzi ya Kiislamu yanayoendelea katika eneo nyeti la Mashariki ya Kati.
Gazeti hilo limesema kuwa mapinduzi hayo yamebadili kimsingi hali ya kiusalama katika eneo hili na kuufanya utawala haramu wa Israel kutengwa kabisa. Kurier limeendelea kuhoji kuwa Wazayuni wataendelea kuuvumilia utawala wao hadi lini kwa kutilia maanani kwamba utawala huo wenyewe unakabiliwa na matatizo chungu nzima ya ndani. Gazeti hilo limekumbusha kwamba utawala haramu wa Israel hauna uwezo wa kukabiliana na matukio ya eneo na hivyo kuupelekea kutengwa kabisa kieneo na kimataifa. 860401
captcha