IQNA

Askari wa Saudia washambulia waombolezaji wa Imam Swadid (as)

15:17 - September 25, 2011
Habari ID: 2192924
Askari wa Saudi Arabia na Bahrain wamewashamblia waombolezaji wa Bahrain waliokuwa wakiomboleza kuawa shahidi Imam Ja'ffar as-Swadiq (as) mmoja wa Watu wa Nyumba ya Mtume Mtukufu (saw) na hivyo kuamsha hasira ya wafuasi wa Ahalul Bait (as) katika nchi hizo.
Maombolezo ya kuhuisha kumbukumbu hiyo chungu yalifanyika katika miji mbalimbali ya Mashia nchini Saudia ikiwemo ya Qatif, Umm Hamam, Saihat na pia katika sehemu za mji wa Madina. Kikao muhimu cha maombolezo ya wanawake kilifanyika katika Kituo cha Hauraa mjini Hamam ambapo washiriki walikumbusha nafasi muhimu aliyokuwa nayo Imam Swadiq (as) katika kueneza mafundisho ya Uislamu halisi katika mazingira magumu ya maisha yake. Maombolezo mengine muhimu ya kukumbuka kifo cha Imam Swadiq (as) yalifanyika katika mji wa Qatif ambapo Sheikh Abdul Hayy Aal Qambar alihutubia waombolezaji. Maombolezo kama hayo yalifanyika katika Msikiti wa Imam Jawad (as) mjini Saihat ambapo Hujjatul Islam wal Muslimeen Ali Aal Suleis Yahya alizungumza. 866434
captcha