IQNA

Amnesty International yalaani hatua za ukandamizaji za utawala wa Saudia

15:21 - September 25, 2011
Habari ID: 2192926
Shirika la Msamaha Duniani, Amnesty Interational limekosoa vikali hatua za utiwaji nguvuni na ukandamizaji unaofanywa na utawala wa Saudi Arabia dhidi ya watu wanaopigania marekebisho ya kisiasa nchini humo.
Shirika hilo limesema kuwa lina wasiwasi mkubwa kuhusiana na kuhukumiwa visivyo Walid Abul Kheir, mwanaharakati mashuhuri wa kupigania haki za binadamu wa Saudia ambaye hivi karibuni alitaka kuhitimishwa kwa mfumo wa utawala wa kifalme wa Aal Saud.
Likimnukuu mwanaharakati huyo, Amnesty International imesema kuwa utawala wa Saudia unamtia mbaroni kila mtu au kundi linaloonyesha kutoridhishwa na utawala wa nchi hiyo ili kuepusha kutokea nchini humo kwa mgogoro wa kisiasa kama ile inayoonekana katika nchi nyingine za kidikteta katika nchi za Kiarabu.
Imeongeza kuwa hatua hiyo ya ukandamizaji sio ngeni kwa watawala wa Saudia kwani huko nyuma wamekuwa wakikandamiza na kuwatia nguvuni wanaharakati wanaolalamikia hali ya kisiasa ya nchi hiyo na wanaotaka marekebisho yafanyike haraka iwezekanavyo. 866210
captcha