IQNA

Hizbullah yalaani mauaji ya kigaidi ya Karbala

15:54 - September 26, 2011
Habari ID: 2193701
Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imelaani milipuko ya kigaidi iliyotokea jana katika mji mtakatifu wa Karbala na kuitaja jinai hiyo kuwa inaoana na maslahi ya wavamizi wa Kimarekani nchini Iraq.
Taarifa iliyotolewa leo na Hizbullah imesema kuwa magaidi watenda jinai wangali wanafanya mauaji dhidi ya wanawake na watoto wa Iraq na kuharibu mali ya umma katika miji mitakatifu hususan Karbala.
Taarifa hiyo imesisitiza kwamba jinai zinazofanywa mtawalia katika kipindi hiki cha kukaribia wakati wa kuondoka askari wavamizi wa Marekani nchini Iraq zinazusha maswali mengi kuhusu wahusika halisi wa vitendo hivyo vya kigaidi.
Hizbullah imelaani jinai hiyo na kuitaja kuwa inadhamini maslahi ya wavamizi wa Kimarekani na vibaraka wao wanaofanya jitihada za kuzuia kuondoka askari wa Marekani katika ardhi ya Iraq.
Sambamba na kutoa mkono wa pole kwa familia zilizopatwa na msiba za Iraq, Hizbullah imewataka Wairaqi kutowapa fursa wavamizi wa Kimarekani na vibaraka wao na kushirikiana kwa ajili ya kuzima njama zao.
867572


captcha