Farzin Ahmad, mwanachama wa Taasisi ya Kiislamu ya Nepal, ameuawa kwa kupigwa risasi na magaidi wawili waliokuwa wamepanda kwenye pikipiki alipokuwa akitoka msikitini baada ya kuswali msikitini humo huko katika mji mkuu, Katmandu.
Kiongozi huyo wa Waislamu ameuawa shahidi alipokuwa njiani kurejea nyumbani kwake. Hii ni mara ya pili kwa wanachama wa taasisi iliyotajwa ya Kiislamu kulengwa na magaidi.
Polisi wanasema kuwa wameanzisha uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo ya kigaidi. Inasemekana kuwa hali ya Waislamu wa Nepal imeendelea kuwa mbaya katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.
Hivi karibuni Wahindu walio na misimamo ya chuki na taasubi dhidi ya Uislamu wamekuwa wakishirikiana na vyama vyenye misimamo mikali vya Nepal kwa lengo la kukandamiza Waislamu wa mji wa Nepal Ganj ambao ni moja ya miji iliyo na wakazi wengi wa Kiislamu. Kwa mujibu wa katiba ya Nepal, ni Wahindu tu ndio walio na ruhusa ya kuhubiri hadharani dini yao ya kuabudu masanamu. 868590