IQNA

Wazayuni kuzuia Waislamu kuingia kwenye Haram ya Nabii Ibrahim (as)

14:38 - September 28, 2011
Habari ID: 2195077
Utawala Haramu wa Israel umechukua hatua ya kupiga marufuku na kuwazuia Waislamu kuingia kwenye Haram ya Nabii Ibrahim (as) siku za Alkhamisi na Ijumaa zijazo kwa kisingizio cha kuwadia mwaka mpya wa Kiibrania.
Utawala huo umetoa taarifa ukitangaza kwamba Waislamu hawataruhusiwa kukaribia eneo hilo takatifu lililoko katika mji wa al-Khalil katika siku mbili zilizotajwa kwa mnasaba wa kuadhimishwa sherere za mwaka mpya wa Kiyahudi.
Wazayuni wamezidisha jinai na mauaji dhidi ya Waislamu wasio na hatia katika mji huo ambapo hivi karibuni mhanga wa mauaji hayo alikuwa mtoto aliyekuwa na umri wa miaka minane.
Wapalestina wengi wamehudhuria mazishi ya mtoto huyo na kudhihirisha hasira yao dhidi ya walowezi na magaidi wa Kizayuni.
Haram ya Nabii Ibrahim iliyoko katikati ya mji wa al-Khalil kusini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni eneo la pili kwa utukufu katika ardhi za Palestina baada ya Msikiti wa al-Aqsa. Kwa kuteka majengo matano muhimu na maeneo mengine kadhaa ya makazi yanayoizunguka Haram hiyo, utawala haramu wa Kizayuni umeligeuza eneo hilo takatifu kuwa la kijeshi. 868639
captcha