IQNA

Kikao cha Muungano wa Idhaa na Televisheni za Kiislamu chamalizika

11:58 - September 29, 2011
Habari ID: 2195399
Sherehe ya kufungwa rasmi kikao cha tano cha Muungano wa Idhaa na Televisheni za Kiislamu ilifanyika alasiri ya jana Jumatano katika ukumbi wa Taasisi ya Idhaa na Televisheni ya Jamhuri ya Kiislamu mjini Tehran.
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na mkuu wa taasisi iliyotajwa Sayyid Izzatullah Dharghami pamoja na wajumbe mbalimbali wa nchi zilizoshiriki katika kikao hicho.
Washindi wa vipindi bora zaidi vilivyowasilishwa kwa kamati maalumu za uchunguzi wa vipindi kabla ya kufanyika kikao hicho, walitunukiwa zaidi nono katika sherehe hiyo. 869535
captcha