IQNA

Ndege za utawala wa Israel zashambulia Gaza

16:57 - October 01, 2011
Habari ID: 2196697
Ndege za kivita za Israel siku ya Alkhamisi zilishambulia kinyama maeneo ya Ukanda wa Gaza na kuharibu vibaya moja ya majengo yanayomilikiwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas.
Jeshi la utawala huo lilitangaza kutekeleza shambulio hilo na kusema kuwa lililenga miongoni mwa maeneo mengine, jengo la harakati ya Hamas katika eneo la al-Maghazi.
Wakati huohuo Kamati ya Utendaji ya Chama cha Ukombozi wa Palestina kinachoongozwa na Mahmoud Abbas ambaye hivi karibuni aliwasilisha katika Umoja wa Mataifa pendekezo la kuundwa nchi huru ya Palestina, imekataa pendekezo lililotolewa hivi karibuni na Kamati ya Pande Nne la kufanya mazungumzo eti ya amani na utawala haramu wa Israel. Kamati hiyo ya Palesina imesema kwamba haitafanya mazungumzo ya aina yoyote na utawala huo hadi pale itakapohisi kwamba una nia nzuri ya kufanya mazungumzo kwa lengo la kufikiwa natija ya kuridhisha pande mbili. 870131
captcha