Mkutano wa 5 wa kimataifa la Intifadha ya Palestina umefunguliwa hapa mjini Tehran mapema leo kwa hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka zaidi ya nchi 100 duniani.
Mkutano huo wa siku mbili ambao umeandaliwa na Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unazishirikisha zaidi ya kamati 70 za Bunge kutoka nchi mbalimbali, maulamaa, shakhsia, wawakilishi wa vyama vya kisiasa pamoja na viongozi wa Kipalestina.
Aidha maspika wa mabunge ya nchi kadhaa za ulimwengu wa Kiislamu wanashiriki katika mkutano huo.
Mkutano wa mara hii unafanyika huku Wapalestina wakiwa wamewasilisha katika Umoja wa Mataifa, ombi la kutaka nchi yao itambuliwe rasmi kuwa ni miongoni mwa nchi huru duniani. Habari zaidi kuhusiana na mkutano huo itakujieni baadaye. 870754