Milod Abu Dia amesema kuwa kaburi hilo lina mabaki ya maiti 11 za wapiganaji wa Baraza la Mpito la Libya.
Amesema kuwa kaburi hilo liligunduliwa jana katika eneo la al Asabia likiwa na mabaki ya maiti 11 zilizotupwa kwenye visiwa viwili. Abu Dia ameongeza kuwa mabaki ya maiti nyingine ya mwanamapinduzi wa Libya yaligunduliwa jana katika eneo la kutupa taka katika eneo hilo hilo la al Asabia.
Makubri mengi ya umati yameundliwa nchini Libya tangu baada ya kuanza mapinduzi ya wananchi aliyomlazimisha dikteta wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi akimbilie sehemu isiyojulikana. 871031