Taarifa hiyo inawataka wananchi kushiriki kwenye maandamano hayo wakiwa kwenye magari yao. Muungano huo umetangaza kuwa lengo la kufanya maandamano hayo kwa mbinu hiyo ni kuvuruga shughuli za kawaida katika maeneo ya kibiashara ya mji mkuu ikiwa ni ishara ya kulalamikia hukumu za kidhulma zilizotolewa hivi karibuni na watawala wa nchi hiyo dhidi ya watuhumiwa wa maandamano ya hivi karibuni nchini.
Muungano huo wa vijana pia umetaka maandamano mengine kama hayo yafanyike siku ya Alkhamisi ijayo kwa ajili ya kuvuruga shughuli za kawaida katika maeneo wanayoishi wanadiplomasia wa kigeni nchini humo.
Muungano huo wa Vijana wa Februari 14 umeyataka mashirika ya kibiashara kutoshirikiana na utawala dhalimu wa Aal Khalifa na kusisitiza kwamba mazingira mazuri ya kibiashara hayatapatikana nchini hadi wakati mfumo nzuri wa utawala wa wananchi utakapoanzishwa nchini humo.
Vijana hao pia wamewataka wananchi wa eneo la an-Nuweidarat kushiriki kwenye maandamano yaliyopangwa kufanyika katika eneo hilo siku ya Ijumaa dhidi ya utawala wa Bahrain. 872176