Gazet la al Intiqad linalochapishwa Lebanon limeandika kuwa Wazayuni wenye misimamo mikali wamechoma moto msikiti huo mepema leo na kuharibu sehemu yake kubwa.
Kabla ya kuchoma moto msikiti huo, walowezi hao wa Kizayuni waliandika nara za kibaguzi katika kuta za eneo hilo la ibada.
Ripoti zinasema kuwa baada ya kuchomwa moto msikiti huo kulitokea mapigano makali baina ya wakazi wa kijiji hicho na askari wa utawala ghasibu wa Israel.
Walowezi wa Kiyahudi wamezidisha mashambulizi na hujuma dhidi misikiti ya Waislamu huko Palestina. 872472