Harakati ya Septemba 9 imetangaza kuwa mkusanyiko huo utafanyika Alkhamisi ijayo.
Msemaji wa harakati hiyo Ibrahim Fadhl amesisitiza katika kikao kilichohudhuriwa na harakati na vyama 21 vya siasa mjini Cairo juu ya udharura wa kushiriki makundi yote ya wananchi katika maandamano hayo na kuwataka watu kushiriki kupitia mitandao ya kijamii kama Facebook.
Taarifa ya Harakati ya Septemba 9 ambayo ipewa jina la 'taifa linataka kufutwa mkataba wa Camp David' imesema matakwa muhimu ya wananchi ni kutoutambua rasmi utawala ghasibu wa Israel, kufutwa mikataba yote ya Misri na utawala huo bandia, kufungwa ubalozi wa Israel mjini Cairo na kufukuzwa balozi wake nchini Misri.
Mkataba wa Camp David ulitiwa saini mwaka 1979 kati ya rais wa wakati huo wa Misri Anwar Sadat na Waziri Mkuu wa wakati huo wa utawala ghasibu wa Israel Menachem Begin chini ya usimamizi wa rais wa wakati huo wa Marekani. 872218