Taarifa hiyo imesema kuwa inasikitisha kuona vitendo vya uvunjiwaji heshima matukufu ya Kiislamu na Kikristo vinatekelezwa mara kwa mara na walowezi wa Kizayuni hali ya kuwa jamii inayodai kutetea haki za binadamu ya nchi za Magharibi imekaa kimya na kutochukua hatua yoyote ya kukabiliana navyo.
Taarifa hiyo imesema kitendo cha hivi karibuni cha kuteketezwa msikiti pamoja na nuskha za Qur'ani Tukufu na vilevile kuandikwa nara za matusi dhidi ya Uislamu na Waislamu kwenye kuta za msikiti huo kwa mara nyingine tena kinaweka wazi utambulisho wa ubaguzi wa utawala ghasibu wa Israel.
Hizbullah imesema kuwa kitendo hicho cha aibu kinabainisha wazi kwamba walowezi wa Kizayuni wanaokalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina hawana haya ya kutekeleza vitendo hivyo vya kijinai na kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu kwa sababu wanatambua vyema kwamba utawala haramu wa Israel unawaunga mkono kwa hali na mali. Imeongeza kuwa jambo hilo ni hatari kubwa kwa maeneo mengine matukufu ya Kiislamu katika ardhi za Palestina na hasa Msikiti Mtukufu wa al-Aqsa. 872974