Kwa mujibu wa gazeti la al-Intiqad la nchini Lebanon, hayo yamesemwa na Leon Panetta, Waziri wa Ulinzi wa Marekani na kuongeza kwamba utawala huo wa Kizayuni hauko katika hali nzuri kwa kutilia maanani mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea katika Mashariki ya Kati.
Panetta ametahadharisha dhidi ya kuendelea kutengwa zaidi utawala huo katika siku zijazo na kusisitiza kuwa utawala huo unapasa kuimarisha juhudi zake za kuboresha uhusiano wake ulioharibika na nchi za Uturuki na Misri.
Amesema si kwa maslahi ya Israel kuendelea kutengwa katika eneo muhimu la Mashariki ya Kati. Akiashiria kwa njia isiyo ya moja kwa moja kujizatiti kwa silaha utawala wa Tel Aviv, Panetta amesema kwamba usalama wa kweli unapatika tu pale zilaha zipounganishwa na juhudi za kidiploamasia.
Waziri huyo wa ulinzi hivi karibuni alifanya safari katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel ambapo alionana na kuzungumza na viongozi wa utawala huo haramu. 872661