IQNA

Waislamu wazuiwa na Wazayuni kuingia katika Msikiti wa Nabii Ibrahim (as)

16:18 - October 08, 2011
Habari ID: 2199879
Tokea siku ya Jumanne asubuhi aslkari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamekuwa wakiwazuia waumini wa Kiislamu kuingia katika Msikiti wa Nabii Ibrahim (AS) kwa ajili ya kutekeleza ibada zao.
Akibainisha suala hilo, Zeid al- Jabbari, mkuu wa masuala ya wakfu ya Waislamu katika mji wa al-Khalil katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan amesema kuwa askari usalama wa utawala haramu wa Israel walifunga milango yote ya kuingilia kwenye msikiti huo siku ya Jumanne iliyopita na kisha kuwaruhusu Mayuhudi kuingia humo kwa lengo la kutekeleza sherehe zao za Yom Kippur.
Utawala wa Israel umetangaza kuwa ni Mayahudi tu ndio watakaoruhusiwa kuingia msikitini humo hadi kufikia siku ya Jumamosi tarehe 8 Oktoba.
Msikiti wa Nabii Ibrahim ambao una historia ya miaka 1000, unachukuliwa kuwa eneo muhimu na takatifu la ibada kwa dini zote za Kiislamu, Kiyahudi na Kikristo. Msikiti huo ni wa pili kwa utukufu baada ya Msikiti wa al-Aqsa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Israel.
Msikiti huo uligawanywa katika sehemu mbili ya Waislamu na Mayahudi kufuatia mauaji ya umati yaliyofanywa na Mayahudi dhidi ya Waislamu mwaka 1994 ambapo watu 29 waliuawa na wengine 159 kujeruhiwa. Tokea wakati huo hadi sasa Mayahudi wamekuwa wakikanyaga wazi haki za Waislamu kutokana na uungaji mkono wa moja kwa moja wa utawala wa Tel Aviv.
Adhana imepigwa marufuku katika msikiti huo katika nyakati za alasiri na usiku. 873915
captcha