IQNA

Mambo yanayofanana kati ya Uislamu na Ukristo kuchunguzwa

16:25 - October 08, 2011
Habari ID: 2200998
Masuala yanayofanana kati ya Uislamu na Ukristo yanachunguzwa katika kikao kinachofanyika hii leo Jumamosi huko mjini Lyon, Ufaransa.
Kwa mujibu wa tovuti ya saphirnews, Jumuiya ya Wakristo na Waislamu ya Walebanon wanaoishi Lyon imeamua kufanya kikao hicho kwa lengo la kusisitiza masuala yanayofanana kati ya dini mbili hizi za mbinguni kama njia ya kuimarisha mazungumzo ya kidini kati ya pande hizo.
Waandaaji wa kikao hicho wamesema kuwa kitasaidia pia kuwasihi wafuasi wa dini mbili hizo waishi pamoja kwa amani bila kuvutana kuhusiana na masuala ya kidini na kijamii.
Waandaaji wa kikao hicho pia wanapanga kufanya vikao vingine kama hicho katika miji ya Paris na Nice. 875259
captcha