Ikiwa ni katika kuendeleza siasa zake zilizo dhidi ya Uislamu, mahakama moja ya Baku mji mkuu wa Azerbaijan imemhukumu kifungo cha miaka 12 jela Mausum Swamdav, Kiongozi wa chama cha Kiislamu cha nchi hiyo.
Mahakama hiyo ilitoa hukumu hiyo jana Ijumaa dhidi ya viongozi kadhaa wa chama hicho cha Kiislamu cha Jamhuri ya Azerbaijan kwa kuwapa vifungo vya kati ya miaka 10 hadi 12.
Viongozi hao ambao wanapinga vikali siasa za serikali za kuwakandamiza Waislamu na kupinga shughuli za kidini walitiwa nguvuni mwaka uliopita kwa tuhuma za kufanya njama za kuipindua serikali.
Waislamu wa nchi hiyo iliyo na wakazi wengi wa Kiislamu wanalalamikia vikali siasa za serikali za kukandamiza shughuli za kidini katika shule na idara za serikali likiwemo suala la kupiga marufuku vazi la hijabu shuleni. 875353