Obama ameyasema hayo katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa muda wa Tunisia mjini Washington na kuongeza kuwa serikali yake inaunga mkono tajiriba ya kidemokrasia ya Tunia ya sasa.
Hadi kabla ya kung'olewa madarakani utawala wa kidikteta wa Zainul Abidin bin Ali, Barack Obama alikuwa muitifaki mkubwa wa serikali ya dikteta huyo.
Ni vyema kukumbusha kuwa Marekani ilikuwa muitifaki na msaidizi mkubwa wa serikali iliyoondolewa madarakani na wananchi wa Tunisia na misimamo ya sasa ya Obama inaakisi mabadiliko ya kistratijia katika siasa za nje za Marekani kwa shabaha ya kutaka kupora na kuteka nyara mapinduzi ya wananchi. 875693